Mwenye kujuzisha uasi dhidi ya kiongozi anaitwa Khawaarij


Swali: Wale ambao wanaonelea kuwa inajuzu kufanya uasi dhidi ya viongozi wanazingatiwa kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah au Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaalah?

Jibu: Wanazingatiwa ni katika Khawaarij, kama alivyowaita Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni katika wavunjaji na Khawaarij, kama ilivyotajwa katika Hadiyth. Kwa nini tuwaite kuwa ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah? Haya sio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah yanasema mtu asikilize na atii mtawala wa waislamu maadamu hajaamrisha maasi. Ama kuwafanyia uasi, sio katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/Mowalat--1426-11-3_0.mp3
  • Imechapishwa: 05/09/2020