Swali: Maneno Yake Allaah (Ta´ala):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ
“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[1]
yanajumulisha wenye kuacha amri za Allaah kama vile swalah?
Jibu: Ndio, anajumuishwa mwenye kuacha amri na mwenye kutenda makatazo, isipokuwa swalah. Kwa mujibu wa maoni sahihi ni kwamba mwenye kuacha swalah kafiri mwenye ukafiri mkubwa. Hii ndiyo sahihi katika jambo hili. Ama zakaah, swawm na hajj kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona mwenye kuyaacha hayo pasi na kuyakanusha – kwa maana ya kwamba ameyaacha lakini hakanushi kuwa ni wajibu – huyu hakufuru, bali anahukumiwa kuwa miongoni mwa watenda madhambi wakubwa. Lakini mwenye kuacha swalah wanazuoni walikhitalifiana tofauti kubwa. Hata hivyo maoni yenye nguvu na sahihi zaidi ni kwamba mwenye kuacha swalah ni kafiri mwenye ukafiri mkubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Baina ya mtu na shirki na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh).
Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”
Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa nne wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupitia kwa Buraydah (Radhiya Allaahu ´anh).
“Kichwa cha Uislamu na nguzo yake ni swalah.”
Zipo Hadiyth nyengine ikiwa ni pamoja na ile ambayo Maswahabah walikupa kiapo cha utii kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba wasivutane na wenye mamlaka kisha akasmea:
“Isipokuwa muone ukafiri wa wazi, mna dalili ya wazi kutoka kwa Allaah juu yake.”
Imekuja katika tamko jengine:
“… muda wa kuwa wanatekeleza kati yenu swalah.”
Kwa hiyo ikafahamisha kuwa mwenye kuacha swalah amefanya ukafiri wa wazi.
[1] 04:48
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25105/هل-يدخل-تارك-الاوامر-في-ان-الله-لا-يغفر-ان-يشرك-به
- Imechapishwa: 02/02/2025
Swali: Maneno Yake Allaah (Ta´ala):
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ
“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[1]
yanajumulisha wenye kuacha amri za Allaah kama vile swalah?
Jibu: Ndio, anajumuishwa mwenye kuacha amri na mwenye kutenda makatazo, isipokuwa swalah. Kwa mujibu wa maoni sahihi ni kwamba mwenye kuacha swalah kafiri mwenye ukafiri mkubwa. Hii ndiyo sahihi katika jambo hili. Ama zakaah, swawm na hajj kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona mwenye kuyaacha hayo pasi na kuyakanusha – kwa maana ya kwamba ameyaacha lakini hakanushi kuwa ni wajibu – huyu hakufuru, bali anahukumiwa kuwa miongoni mwa watenda madhambi wakubwa. Lakini mwenye kuacha swalah wanazuoni walikhitalifiana tofauti kubwa. Hata hivyo maoni yenye nguvu na sahihi zaidi ni kwamba mwenye kuacha swalah ni kafiri mwenye ukafiri mkubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Baina ya mtu na shirki na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh).
Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”
Ameipokea Imaam Ahmad na watunzi wa nne wa Sunan kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kupitia kwa Buraydah (Radhiya Allaahu ´anh).
“Kichwa cha Uislamu na nguzo yake ni swalah.”
Zipo Hadiyth nyengine ikiwa ni pamoja na ile ambayo Maswahabah walikupa kiapo cha utii kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba wasivutane na wenye mamlaka kisha akasmea:
“Isipokuwa muone ukafiri wa wazi, mna dalili ya wazi kutoka kwa Allaah juu yake.”
Imekuja katika tamko jengine:
“… muda wa kuwa wanatekeleza kati yenu swalah.”
Kwa hiyo ikafahamisha kuwa mwenye kuacha swalah amefanya ukafiri wa wazi.
[1] 04:48
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25105/هل-يدخل-تارك-الاوامر-في-ان-الله-لا-يغفر-ان-يشرك-به
Imechapishwa: 02/02/2025
https://firqatunnajia.com/mwenye-kuacha-swalah-anaingia-ndani-ya-matakwa-ya-allaah/