Mwenye kuacha kufanya Hijrah ni mtenda dhambi kubwa

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amejitenga mbali na waislamu wenye kuishi kati ya washirikina. Muislamu anayeishi katika mji wa Kiislamu pamoja na kuwa anaweza kufanya Hijrah anazingatiwa ni mtenda dhambi kubwa au ni kafiri?

Jibu: Ni mtenda dhambi kubwa. Kwa sababu Allaah amewatishia:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali wamejidhulumu nafsi zao.”

Bi maana watu wenye kuishi pamoja na makafiri:

قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ

Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.”

Bi maana hatukuweza kudhihirisha dini yetu kwa sababu ya makafiri wanatuzuia:

قَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

“Watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa ya wasaa mkahajiri? Basi hao makazi yao yatakuwa ni [Moto wa] Jahannam – na uovu ulioje mahali pa kuishia!” (04:97)

Haya ni matishio. Ni dalili yenye kuonesha kuwa mwenye kuacha kufanya Hijrah, pamoja na kuwa mtu ana uwezo wa kufanya hivo, ni dhambi kubwa na mtu anaguswa na matishio haya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (29) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20%20-%2025%20-%201%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017