Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke mwenye hedhi kusoma Qur-aan ikiwa iko ndani ya simu?

Jibu: Mwenye hedhi, aliye na hadathi kubwa na mwenye janaba hawaruhusiwi kusoma Qur-aan, sawa ikiwa ni ndani ya Kitabu au kimoyoni. Wasisome Qur-aan, sawa ikiwa iko ndani ya kitu na kinachodhihiri ni herufi zake tu kwenye skrini, ndani ya msahafu na kadhalika. Asisome Qur-aan ilihali ana hadathi kubwa mpaka aoge.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13221
  • Imechapishwa: 23/09/2020