Swali: Mwenye hedhi kusoma nyuradi zake na kuirejea kwake Qur-aan.
Jibu: Hapana vibaya kusoma nyuradi. Lakini asisome Qur-aan. Asome nyuradi zake isiyokuwa Qur-aan. Akisoma kutoka katika hifdhi yake hapana vibaya pia kwa mujibu wa maoni sahihi bila ya kugusa msahafu.
Swali: Asome kwa hifdhi?
Jibu: Hapana vibaya akisoma kwa hifdhi yake. Hakuna dalili inayokataza. Muda wa hedhi unarefuka. Sio kama mwenye janaba. Muda wake ni mrefu. Vivyo hivyo kuhusu mwanamke mwenye damu ya uzazi. Akisoma hapana neno kwa mujibu wa maoni sahihi. Lakini asiguse msahafu. Lakini hapana vibaya akihitaji kusoma ndani ya msahafu baadhi ya Aayah nyuma ya kizuizi na nyuma ya vifuko vya mikono.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23535/حكم-قراءة-الحاىض-للقران
- Imechapishwa: 06/02/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)