Swali: Baadhi ya wafasiri wa Qur-aan wanasema kunahitajika dalili kusema kwamba mafuriko yalienea duniani kote. Allaah ametukhabarisha ya kwamba aliwaangamiza watu wa Nuuh kwa gharika. Lakini kusema kuwa hilo lilienea ardhini kote ni jambo linahitaji dalili na uthibitisho?
Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi. Kinachokusudiwa ni kwamba Allaah aliwaangamiza watu wote wa ulimwenguni isipokuwa waliokuwa ndani ya safina. Lakini kusema kuwa hilo lilienea ardhini kote si lazima iwe hivo. Kinachokusudiwa ni kwamba yaliangamizwa yale maeneo yaliyo na wakazi. Ama yale maeneo ambayo hakukuwepo na yeyote inawezekana hakukufikiwa na gharika. Lakini Mola (Jalla wa ´Alaa) ameeleza:
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ
”Hakika Tulimtumiliza Nuuh kwa watu wake akakaa nao miaka elfu kasoro miaka khamsini, basi ikawachukua tufani nao ni madhalimu.”[1]
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ
”Basi Tukamuokoa na watu wa jahazi na tukaifanya kuwa ni alama kwa walimwengu.”[2]
Wengineo hawakusalimika. Wale ambao hawakuwepo ndani ya jahazi waliangamia. Tunamuomba Allaah usalama.
Swali: Haikutajwa kuhusu ardhi:
وَقِيلَ يَا أَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ
”Pakasemwa: ”Ee ardhi! Meza maji yako.”[3]
Bi maana ardhi…
Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi. Kinachokusudiwa ni kwamba ardhi yaliwaenea watu mpaka makafiri mpaka wakaangamia wote. Isipokuwa waliokuwa ndani ya jahazi. Lakini kusema kwamba maji yalienea kila eneo hata kama maeneo hayo hakuna yeyote, Allaah ndiye anayejua zaidi.
[1] 29:14
[2] 29:14
[3] 11:44
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23538/هل-ثبت-ان-طوفان-نوح-عم-الارض-كلها
- Imechapishwa: 06/02/2024
Swali: Baadhi ya wafasiri wa Qur-aan wanasema kunahitajika dalili kusema kwamba mafuriko yalienea duniani kote. Allaah ametukhabarisha ya kwamba aliwaangamiza watu wa Nuuh kwa gharika. Lakini kusema kuwa hilo lilienea ardhini kote ni jambo linahitaji dalili na uthibitisho?
Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi. Kinachokusudiwa ni kwamba Allaah aliwaangamiza watu wote wa ulimwenguni isipokuwa waliokuwa ndani ya safina. Lakini kusema kuwa hilo lilienea ardhini kote si lazima iwe hivo. Kinachokusudiwa ni kwamba yaliangamizwa yale maeneo yaliyo na wakazi. Ama yale maeneo ambayo hakukuwepo na yeyote inawezekana hakukufikiwa na gharika. Lakini Mola (Jalla wa ´Alaa) ameeleza:
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَلَبِثَ فِيهِمْ أَلْفَ سَنَةٍ إِلَّا خَمْسِينَ عَامًا فَأَخَذَهُمُ الطُّوفَانُ وَهُمْ ظَالِمُونَ
”Hakika Tulimtumiliza Nuuh kwa watu wake akakaa nao miaka elfu kasoro miaka khamsini, basi ikawachukua tufani nao ni madhalimu.”[1]
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَصْحَابَ السَّفِينَةِ وَجَعَلْنَاهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ
”Basi Tukamuokoa na watu wa jahazi na tukaifanya kuwa ni alama kwa walimwengu.”[2]
Wengineo hawakusalimika. Wale ambao hawakuwepo ndani ya jahazi waliangamia. Tunamuomba Allaah usalama.
Swali: Haikutajwa kuhusu ardhi:
وَقِيلَ يَا أَرْضُ ابْلَعِي مَاءَكِ
”Pakasemwa: ”Ee ardhi! Meza maji yako.”[3]
Bi maana ardhi…
Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi. Kinachokusudiwa ni kwamba ardhi yaliwaenea watu mpaka makafiri mpaka wakaangamia wote. Isipokuwa waliokuwa ndani ya jahazi. Lakini kusema kwamba maji yalienea kila eneo hata kama maeneo hayo hakuna yeyote, Allaah ndiye anayejua zaidi.
[1] 29:14
[2] 29:14
[3] 11:44
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23538/هل-ثبت-ان-طوفان-نوح-عم-الارض-كلها
Imechapishwa: 06/02/2024
https://firqatunnajia.com/je-imethibiti-kuwa-tufani-ya-nuuh-ilienea-duniani-kote/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)