Swali: Mtu ana kiwango kinachopaswa kutolewa zakaah, lakini yuko na deni ambalo likikadiriwa kupunguza hicho kiwango. Je, atatoa zakaah?

Jibu: Jawabu sahihi ni kwamba deni halizuii kutolewa zakaah. Hata kama mtu ana deni la 100 000 na ana mali ya 200 000, hawambiwi apunguze deni halafu atoe zakaah kwa kilichobaki. Hapana. Anatakiwa atoe zakaah kutokana na mali aliyonayo na deni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atamrahisishia kulilipa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwatuma wakusanyaji wa zakaah kwa watu, nao walikusanya zakaah bila kuuliza kama mtu ana deni au hana. Hitimisho ni kwamba deni halizuii zakaah. Kama mtu ana deni la 100 000 na ana mali ya 100 000 ya fedha taslimu, basi ataitoa zakaah. Deni halizuii.

Swali: Vipi kuhusu nadhiri na kafara ikiwa kulipa nadhiri au kafara kunapunguza kiwango cha wajibu?

Jibu: Vyote havizuii zakaah. Deni, nadhiri wala kafara, hakuna hata kimoja kinachozuia wajibu wa kutolewa zakaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1081/هل-على-المدين-اخراج-زكاة
  • Imechapishwa: 27/01/2026