Swali: Ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi kugusa msahafu pasina kizuizi? Na ni ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi na nifasi kuingia msikitini?
Jibu: Kugusa msahafu pasina kizuizi ni kwamba inajuzu kwa kukosekana dalili sahihi zinazopinga hilo. Ama Kauli Yake (Ta´ala):
لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ
“Hawaigusi isipokuwa waliotwahara.” (56:79)
makusudio hapa ni Malaika. Kama Alivyosema hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika Kitabu Chake Kitukufu:
وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ الشَّيَاطِينُ وَمَا يَنبَغِي لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ
“Na wala hawakuteremka nayo [Qur-aan hii] mashaytwaan na wala haipasi kwao na wala hawawezi.” (26:210)
“Iliyoifasiri Aayah hii vizuri, ni Kauli nyingine ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
كَلَّا إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ فَمَن شَاءَ ذَكَرَهُ فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ بِأَيْدِي سَفَرَةٍ كِرَامٍ بَرَرَةٍ
“Sivyo katu! Hakika hizi ni Ukumbusho. Basi atakaye akumbuke. [Zimeandikwa] katika swahifa zilizokirimiwa. Zimetukuzwa na zimetwaharishwa. [Zinazobebwa] mikononi mwa waandishi, watukufu na watiifu.” (80:11-16)
Na makusudio hapa katika Aayah hii ni Malaika. Hivyo Aayah hii ya al-Waaqi´ah makusudio ni Malaika – na Allaah (Ta´ala) ndiye Mwenye kujua zaidi. Ama mwanamke mwenye hedhi na nifasi kuingia msikitini, sijui kama kuna dalili yoyote katika Kitabu na Sunnah inayokataza hilo. Ama kuhusu Hadiyth:
“Mimi sikuhalalisha msikiti kwa aliye na hedhi na janaba.”
Hadiyth hii ni dhaifu. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamwambia ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):
“Hedhi yako haiko mikononi mwako.”
Na alimwambia tena (´alayhis-Salaam):
“Hapana! Fanya anayopasa kufanya mwenye kuhiji, isipokuwa tu usitukufu kwenye Ka´bah.”
Na katika zama za Mtume kulikowepo mwanamke ambaye anafanya kazi msikitini na anaishi msikitini. Na mwanamke huyu alikuwa kishakuwa mama, anajiwa na yanayowajia wanawake wengine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwahi katu kumwambia:
“Unapojiwa na hedhi, toke nje [ya msikiti].”
Hapa kuna dalili inaonesha kuwa, inajuzu kwa mwanamke kuingia msikitini naye yuko na hedhi au nifasi.
- Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=284
- Imechapishwa: 18/02/2018

Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=284
Imechapishwa: 18/02/2018
https://firqatunnajia.com/mwanamke-mwenye-hedhi-na-nifasi-kushika-msahafu-na-kuingia-msikitini/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)