Mwanamke mwenye hedhi kukaa msikitini na kusikiliza darsa

Swali: Je, inafaa kwake [mwanamke mwenye hedhi na nifasi] kuhudhuria vikao vya elimu na darsa msikitini?

Jibu: Hapana neno – Allaah akitaka. Hadiyth isemayo:

“Mimi siuhalalishi msikiti kwa mwenye hedhi na mwenye janaba.”

ni dhaifu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemwambia ´Aaishah:

“Hedhi yako haiko mikononi mwako.”

Amesema pia:

”Fanya kila kitu isipokuwa kutufu kwenye Ka´bah.”

Ni sawa ikiwa atakaa msikitini na kusikiliza darsa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaaih wa Naswaaih, uk. 80
  • Imechapishwa: 26/08/2020