Kila mtengano ambao unatokea kwa fidia ni Khul´ (kujivua katika ndoa). Haijalishi kitu hata kama itatokea kwa tamko la aina ya talaka. Kwa mfano mwanamme aseme ´nimemtaliki mke wangu kwa fidia ya 1000 SAR. Tunasema kuwa hiyo ni Khul´. Haya ndio yamepokelewa kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa):

“Kila kilichoingiliwa na fidia sio talaka.”

´Abdullaah bin Imaam Ahmad amesema:

“Baba yangu alikuwa anaonelea juu ya Khul´ namna anavyoonelea ´Abdullaah bin ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).”

Bi maana kufutika kwa ndoa, pasi na kujali neno lililotumika, hakuzingatiwi ni talaka.

Haya yanapelekea katika masuala ambayo ni muhimu: mtu akimtaliki mke wake mara mbili kwa nyakati mbalimbali, kisha kukatokea Khul´ yenye tamko aina ya talaka, wale wanachuoni wenye kuona kuwa Khul´ inahesabika ni talaka itazingatiwa ni talaka na mwanamke huyo atatakiwa kutengana na mume huyo. Hiyo ina maana kwamba mwanamke huyo hatokuwa ni halali kwa mwanamme huyo isipokuwa baada ya kuolewa na mume mwengine. Lakini wale wanachuoni wenye kuona kuwa Khul´ ni kufutika kwa ndoa peke yake ingawa yametumika matamshi aina ya talaka, mwanamke huyo atakuwa ni halali kwake kwa kufunga ndoa mpya hata kama ndoa hiyo itakuwa ndani ya eda. Haya maoni ndio yenye nguvu zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumti´ (12/450)
  • Imechapishwa: 05/05/2020