Mwanamke kutazama wachezaji wa mpira wanamme

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kuangalia wachezaji wa mpira na wacheza mieleka kwenye runinga pamoja na kuzingatia kwamba wanavaa mpaka kwenye nusu mapaja?

Jibu: Haitakikani kwake kufanya hivo. Mwanamke anatakiwa kujishughulisha na yenye kumpa faida na awe na heshima na kuitilia umuhimu yale yenye kumpa faida. Vivyo hivyo mwanamme muislamu anatakiwa asipoteze wakati wake na atumie wakati wake kwa yale yanayompa faida katika dini na dunia yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 10/10/2021