Mwanamke kusema katika du´aa ”mja wako” II

Swali: Du´aa ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayosema:

اللّهُـمَّ إِنِّي عَبْـدُكَ، ابْنُ عَبْـدِكَ، ابْنُ أَمَتِـكَ نَاصِيَتِي بِيَـدِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤكَ، أَسْأَلُـكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ، سَمَّـيْتَ بِهِ نَفْسَكَ، أِوْ أَنْزَلْتَـهُ فِي كِتَابِكَ، أَوْ عَلَّمْـتَهُ أَحَداً مِنْ خَلْقِـكَ، أَوِ اسْتَـأْثَرْتَ بِهِ فِي عِلْمِ الغَيْـبِ عِنْـدَكَ، أَنْ تَجْـعَلَ القُرْآنَ رَبِيـعَ قَلْبِـي، وَنورَ صَـدْرِي، وجَلَاءَ حُـزْنِي، وذَهَابَ هَمِّـي

”Ee Allaah! Hakika mimi ni mja Wako, mwana wa mja Wako, mwana wa mjakazi Wako, utosi wangu uko mikononi Mwako, yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako, ni adilifu kwangu unihukumu kwayo, nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako; ulilojiita kwalo Mwenyewe, uliloliteremsha katika Kitabu Chako, ulilomgunza nalo yoyote katika viumbe Vyako, ulilolificha katika elimu ya ghaibu Kwako: nakuomba uifanye Qur-aan kuwa ni uhuisho wa moyo wangu, nuru ya kifua changu na ufumbuzi wa  huzuni yangu.”[1]

Mwanamke aseme nini anapotaka kuomba du´aa hii?

Jibu: Sijui kitu kuhusu hilo. Lakini hapana vibaya akisema:

إني أمَتُك، بِنْتُ عبدك

“Mimi ni mjakazi wako na msichana wa mja wako.”

Ni sawa pia akisema kama ilivyokuja; yeye ni mja kama mwanaume alivo mja.

[1] Ahmad (01/391). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23239/ماذا-تقول-المراة-في-دعاء-اللهم-اني-عبدك
  • Imechapishwa: 13/12/2023