Kumtakia rehema anayepiga chafya zaidi ya mara mbili

Swali: Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo bwana mmoja alichemua mara mbili akamwambia:

يرحمك الله

“Allaah akurehemu.”

Mara ya tatu akamwambia:

الرجل مزكوم

“Bwana huyu ana mafua.”

Jibu: Akimuhimidi Allaah aambiwe:

يرحمك الله

“Allaah akurehemu.”

Haijalishi kitu hata kama atamwambia kuwa ana mafua.

Swali: Aendelee kumwambia:

يرحمك الله

“Allaah akurehemu.”?

Swali: Aambiwe hivo ikiwa atamuhimidi Allaah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23236/حكم-تشميت-العاطس-المزكوم-بعد-مرتين
  • Imechapishwa: 13/12/2023