Mwanamke kulipa siku zake za Ramadhaan bila mume wake kujua

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwanamke anayefunga siku mbili bila ya mume wake kutambua pamoja na kujua ya kwamba funga hii ilikuwa ni ulipaji wa deni la mwezi wa Ramadhaan iliyobarikiwa. Wakati alipokuwa afunga aliona aibu kumweleza mume wako juu ya hilo. Ikiwa haijuzu analazimika kwake kutoa kafara?

Jibu: Ni wajibu kwa mwanamke kulipa siku anazodaiwa za Ramadhaan hata kama mume wake hatojua. Haikushurutishwa kupata idhini kutoka kwa mume wake juu ya kufunga swawm ambayo ni wajibu. Swawm ya mwanamke huyu aliyetajwa ni sahihi.

Kuhusu swawm isiyokuwa ya wajibu haifai kwa mwanamke kufunga ilihali mume wake hakusafiri isipokuwa baada ya kupata idhini yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemkataza mwanamke kufunga na mume wake hakusafiri isipokuwa kwa kupata idhini yake mbali na Ramadhaan[1].

[1] al-Bukhaariy (5195), Muslim (1026), at-Tirmidhiy (782) na wengineo

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: : Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/353)
  • Imechapishwa: 22/06/2017