Swali: Nini maana ya:

”Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake.”[1]?

Jibu: Ni kwa minajili ya matishio. Ni kama mfano wa Hadiyth za makemeo:

”Hatoingia Peponi anayekata kizazi.”

”Hatoingia Peponi mbea.”

Yote haya ni makemeo na matishio. Haina maana kuwa ni makafiri, hapana.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona; wanaume walio na bakora kama mkia wa ng´ombe ambazo wanawapiga kwazo watu, na wanawake waliovaa vibaya, uchi, waliopinda na wanaopindisha wengine. Vichwa vyao ni kama nundu ya ngamia. Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake. Harufu yake inapatikana umbali wa kadhaa na kadhaa.” (Muslim (2128) na Ahmad (2/356).)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24812/معنى-لا-يدخلن-الجنة-ولا-يجدن-ريحها
  • Imechapishwa: 20/12/2024