Swali: Ipi hukumu ya mwanamke kukaa eda nje ya nyumba ya mume wake?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kukaa eda juu ya mumewe nje ya nyumba ya mume wake ambayo imekuja khabari naye yuko humo, kama tulivyosema asitoke katika nyumba aliyomo ambapo amekufa mume wake naye yuko humo isipokuwa tu kwa dharurah. Lakini kwa mfano kapata khabari ya kufa mume wake naye yuko kwa daktari, hapa hatuwezi kusema akae eda hospitali, hapana. Atakaa eda nyumbani kwake, atarudi kwake alipokuwa. Hali kadhalika akijiwa na khabari naye yuko kwa nyumba ya jirani yake, akajiwa na khabari kuwa mumewe amefariki. Hatusemi akae eda kwa hiyo nyumba ya jirani. Kimsingi ni kuwa ametoka nyumbani kwake. Atarudi nyumbani kwake na atabaki humo muda wote wa eda mpaka uishe.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://olamayemen.al3ilm.net/Default_ar.aspx?ID=2008
  • Imechapishwa: 22/01/2023