Swali: Wakati nilipooa familia ya mwanamke ilinishurutishia kumwacha asafiri na kaka yake. Nikakubali shati hiyo. Lakini baada ya ndoa nikaonelea kuwa ni bora kutoenda na nikawa nimekataa yeye kwenda. Nikasikia ya kwamba napata dhambi na Muislamu wako kwa masharti wanayowekeana…

Jibu: Masharti yao sahihi, ndio. Sharti hii sio sahihi. Muislamu wako kwa masharti ambayo ni sahihi. Lakini Hadiyth inasema mwishoni:

“… isipokuwa sharti inayohalalisha haramu au inayoharamisha halali.”

Sharti hii inahalalisha haramu; kusoma nje, mwanamke kutoka nyumbani na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mqirwani–14340317.mp3
  • Imechapishwa: 18/06/2015