Mwanamke anapata dhambi kwa kuswali na suruwali?

Swali: Wanawake wengi wamepewa mtihani leo wa kuvaa suruwali na wanaswali nazo. Je, swalah yake inakubaliwa na Swalah yake ni sahihi mguu wake ukionekana wakati wa Swalah?

Jibu: Mguu wake ukionekana swalah yake sio sahihi kwa kuwa [mguu ni] ´Awrah. Kuhusiana na kuswali kwake na suruwali anapata dhambi kwa kufanya hivo. Lakini hata hivyo swalah yake ni sahihi maadamu suruwali hiyo inafunika ´Awrah yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (80) ttp://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir_08_03_1433.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020