Mwanamke ameavya mimba ya miezi miwili

Swali: Mwanamke aliavya mimba ya miezi miwili zaidi ya miaka ishirini na miwili iliyopita. Leo hawezi kufunga. Hivyo nataka kubadilisha kwa kutoa kiasi cha fedha. Ni aina gani ya swadaqah hiyo? Je, inajuzu kutoa kiasi hicho kwa mtu mmoja au familia masikini inayopokea msaada wa kijamii, kukikabidhi kwa moja ya taasisi za Kiislamu za misaada au kukitoa nje ya nchi kwa kuwa siwezi kukigawa kwa wahitaji?

Jibu: Kiumbe kilicho chini ya miezi minne hakihesabiwi kuwa ni kipomoko na hivyo hakuna lolote juu yake. Kikianguka kabla ya kufikia miezi minne, iwe mwezi mmoja, miwili au mitatu, basi hakuna wajibu wowote. Kinazikwa mahali pazuri na hamna tatizo. Ama kama kiumbe hicho kilikuwa kimepuliziwa roho, basi hapa kuna maelezo. Ikiwa aliavya kwa makusudi, basi anapata dhambi. Anatakiwa kutubu kwa Allaah, ana wajibu wa kutoa kafara na fidia ya sehemu ya kumi ya fidia ya mama yake. Lakini kama kilianguka bila kukusudia, kimetoka kwa bahati mbaya, basi juu yake ni kafara na fidia tu na hana dhambi ikiwa hakukusudia. Ama kilicho chini ya hapo, kabla ya kupuliziwa roho, kikiwa bado ni kipande cha damu au nyama changa, basi hakuna lolote juu yake. Hakuna kafara. Hivyo hakiswaliwi na hakipewi jina. Hakiwi mtoto mpaka roho ipuliziwe ndani yake baada ya kukamilika miezi minne na kuingia mwezi wa tano.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31330/ما-حكم-من-اسقطت-جنينا-عمره-شهران
  • Imechapishwa: 20/10/2025