Mwanamke aliacha swawm idadi nyingi na sasa anataka kulipa

Swali: Mwanamke huyu anasema kuwa mpaka sasa hajalipa deni lake la Ramadhaan kwa miaka mingi. Ni lipi linalomlazimu hivi sasa?

Jibu: Ni lazima kwake kulipa kile kilichompita. Akisema kuwa hajui ni idadi ngapi zilizompita, tunamwambia afanye lililo salama na akadirie halafu baada ya hapo alipe kile kilichompita. Hana juu yake kulisha chakula au kutoa swadaqah kwa mujibu wa maoni yenye nguvu. Kinachomlazimu ni yeye kulipa zile siku ambazo zilizompita.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (25)
  • Imechapishwa: 17/01/2019