Mwanachuoni wa ki-Ibaadhiy akimkufurisha ´Abdullaah bin Sallaam II

´Abdullaah bin Sallaam ni myahudi ambaye alichelewa kuingia katika Uislamu na akaeneza ndani yake I´tiqaad za kiyahudi. Huyu ndiye ´Abdullaah bin Sallaam ambaye amesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وَمِنَ اللَّيْلِ فَتَهَجَّدْ بِهِ نَافِلَةً لَّكَ عَسَىٰ أَن يَبْعَثَكَ رَبُّكَ مَقَامًا مَّحْمُودًا

“Amka katika sehemu ya usiku uswali – ni ziada ya Sunnah kwako – kwani huenda Mola wako akakuinua cheo kinachosifika.”[1]

Maana yake ni kwamba itapofika siku ya Qiyaamah basi ataletwa Mtume wenu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kukalishwa mbele ya Allaah juu ya Kursiy Yake.”[2]

[1] 17:79

[2] al-Haakim (05/568), Ibn Abiy ´Aaswim (786), al-Khallaal katika “as-Sunnah” yake, uk. 209 na ad-Dhahabiy (191).

  • Mhusika: Zakariyyah bin Khaliyfah al-Mahramiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Balsam ash-Shaafi´iy fiy Tanziyh-il-Baariy, uk. 44
  • Imechapishwa: 24/01/2019