Swali: Wakati tulipofika kwenye mlango wa hedhi daktari kwenye chuo kikuu alisema tuuache kwa kuwa sio muhimu kwa nisba yetu na wala hakutushereheshea. Unatunasihi nini?

Jibu: Nendeni kwa mudiri wa kitivo na mumweleze kuwa amewakatishia selebasi. Mudiri wa kitivo ndio atayemshughulikia. Hana khiyari ya kufanya atakacho. Haifai kwake kufuta na kuthibitisha anachotaka. Hana khiyari ya kufanya atakacho. Hili ni jukumu kwenye dhimma yake ambalo analazimika kulitekeleza. Haifai kwake kujiamulia atakavyo.

Hedhi haiwahusu? Inawahusu wa kina nani sasa? Hedhi haiwahusu wanafunzi? Ni yupi atayejifunza hukumu za hedhi? Wao ndio wanaojibu maswali ya watu na ya wanawake. Ni hukumu ya Kishari´ah. Allaah ameweka katika Shari´ah hukumu zinazohusiana na hedhi. Huyu anachukia hedhi na hukumu za hedhi? Hili ni tatizo. Huyu asli ni mwalimu asiyefaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (7) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–15041434.mp3
  • Imechapishwa: 18/12/2016