Mwalimu anamtaka mwanafunzi ampe udhuru japo wa uongo

Swali: Nilichelewa mtihani wa mwezi. Nikamuomba mwalimu kurudi mtihani huo tena ambapo akakataa isipokuwa kwa udhuru. Nikamwambia kwamba mimi sina udhuru wowote labda nikudanganye. Akanijibu kwamba muhimu mimi nimpe udhuru haijalishi kitu hata kama ni uongo na kwamba atayenihukumu ni Allaah. Nimejaribu sana lakini hata hivyo amekataa isipokuwa kwa kumpa udhuru ijapokuwa ni kusema uongo. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Hapana, usiseme uongo. Kusema uongo ni haramu. Haikuvuliwa isipokuwa katika hali tatu na hali hii haingii ndani; mtu anapozungumza na mke wake, vitani na kusuluhisha kati ya watu. Akikinaika ni vizuri. Vinginevyo usiseme uongo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 29/12/2018