Mume wangu haswali mkusanyiko msikitini, nifanye nini?

Swali: Mume wangu swalah nyingi za mkusanyiko zinampita msikitini. Nimemnasihi sana ila haitikii. Nifanye nini?

Jibu: Endelea kumnasihi. Huenda Allaah akamuongoza. Isitoshe, watake msaada watu ambao wanaweza kumuathiri miongoni mwa jamaa zake, ndugu zake na jirani zake wamnasihi. Huenda Allaah akamuongoza. Usimuache na ukakata tamaa. Usikate tamaa juu ya kuongoka kwake au ukaacha kumnasihi. Mwanamke huyo yuko na ujira na yuko juu ya kheri. Huku ni kuamrisha mema na kukataza maovu na ni kumtoa mume wake katika maangamivu haya. Aendelee nae huenda Allaah akamuongoza. Watake msaada watakaokusaidia miongoni mwa jamaa zake au marafiki zake ili wamnasihi.

Check Also

Mwanamke kujibu maswali ya kidini

Swali: Je, mwanamke anaweza kujibia swali alilosikia au kulisoma? Jibu: Ndio, ikiwa yuko na elimu. Wakeze …