Swali: Ikiwa nimeoa mwanamke mwalimu, je, nina haki ya kuchukua mshahara wake kwa ridhaa yake kwa sababu ya haja na maslahi ya wote wawili, kama kujenga nyumba kwa mfano, bila kumpa hati ya kuthibitisha kile nilichochukua, naye hakuniomba hilo ilihali mimi pia nina kazi na ninapokea mshahara wa kila mwezi?
Jibu: Hakuna ubaya kwako kuchukua mshahara wa mke wako kwa ridhaa yake ikiwa ni mwenye akili timamu. Vivyo hivyo kila kitu anachokupa kwa njia ya kusaidia. Hapana vibaya kwako kukipokea ikiwa amekitoa kwa moyo wake wote na akiwa ni mwenye akili timamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَّرِيئًا
”Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa kutaka kwao wenyewe, basi kuleni kwa kufurahia na kunufaika.”[1]
Na hata kama itakuwa bila hati ya maandishi, basi hakuna ubaya. Lakini ikiwa atakupa hati juu ya hilo, basi hilo ni la tahadhari zaidi ikiwa una khofu ya jambo kutoka kwa familia yake au jamaa zake au una khofu ya yeye kurejea madai yake.
[1] 04:04
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/43)
- Imechapishwa: 18/03/2026
Swali: Ikiwa nimeoa mwanamke mwalimu, je, nina haki ya kuchukua mshahara wake kwa ridhaa yake kwa sababu ya haja na maslahi ya wote wawili, kama kujenga nyumba kwa mfano, bila kumpa hati ya kuthibitisha kile nilichochukua, naye hakuniomba hilo ilihali mimi pia nina kazi na ninapokea mshahara wa kila mwezi?
Jibu: Hakuna ubaya kwako kuchukua mshahara wa mke wako kwa ridhaa yake ikiwa ni mwenye akili timamu. Vivyo hivyo kila kitu anachokupa kwa njia ya kusaidia. Hapana vibaya kwako kukipokea ikiwa amekitoa kwa moyo wake wote na akiwa ni mwenye akili timamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَإِن طِبْنَ لَكُمْ عَن شَيْءٍ مِّنْهُ نَفْسًا فَكُلُوهُ هَنِيئًا مَّرِيئًا
”Lakini wakitoa chochote wenyewe katika mahari yao kwa kutaka kwao wenyewe, basi kuleni kwa kufurahia na kunufaika.”[1]
Na hata kama itakuwa bila hati ya maandishi, basi hakuna ubaya. Lakini ikiwa atakupa hati juu ya hilo, basi hilo ni la tahadhari zaidi ikiwa una khofu ya jambo kutoka kwa familia yake au jamaa zake au una khofu ya yeye kurejea madai yake.
[1] 04:04
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/43)
Imechapishwa: 18/03/2026
https://firqatunnajia.com/mume-kuchukua-kutoka-kwenye-mshahara-wa-mke-wake/