Swali: Mwanamke huyu kutoka Ufaransa anasema kuwa aliolewa na mwanaume ambaye anafata Sunnah lakini baba yake mwanamke haridhii msimamo wake na hivyo anamzuia kutokana naye na kuendelea kuishi pamoja naye. Ni ipi nasaha zako kwake?

Jibu: Amekwishaolewa. Baba yake hana mamlaka yoyote kwake. Muda wa kuwa amekwishaolewa na mwanaume ni mwema kwake na amenyooka sawa katika dini na tabia yake, baba yake asimzuie kutokana naye. Haki ya mume inatangulia mbele ya haki ya baba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (45)
  • Imechapishwa: 25/07/2024