Mume anamwita mke majina ya kejeli na ya wanyama

Swali: Ni ipi hukumu ya mume kumwambia mke wake ´ee mnyama` au ´ee mjusi` kwa njia ya mzaha na wanaenda mbali zaidi kwa maneno kama haya? Ni zipi nasaha zako kuhusu matangamano kati ya wanandoa? Je, mume anaridhia kufanyiwa mzaha kwa matamshi kama haya?

Jibu: Allaah (Jalla wa ´Alaa):

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Na kaeni nao kwa wema.”[1]

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Nao wake wana haki kama ambayo [ya waume zao] iliyo juu yao kwa mujibu wa wema; na wanaume wana daraja zaidi juu yao.”[2]

Kama ambavo wewe unachukia mwanamke akuzungumzishe kwa maneno mabaya, basi nawe usimzungumzishe kwa maneno mabaya:

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Nao wake wana haki kama ambayo [ya waume zao] iliyo juu yao kwa mujibu wa wema; na wanaume wana daraja zaidi juu yao.”

وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ

“Na kaeni nao kwa wema.”

Hili linamuhusu mume ambaye tunamnasihi kuacha jambo hili.

Kuhusu mke tunamshauri kufanya subira juu ya hilo. Asipatilize jambo hilo.

[1] 04:19

[2] 02:228

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (02)
  • Imechapishwa: 27/02/2024