05 – Kutoa damu kwa kupiga chuku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Amefungua aliyefanya chuku na aliyefanywa chuku.”

Ameipokea Ahmad na Abu Daawuud kupitia kwa Shaddaad bin Aws.

al-Bukhaariy amesema:

“Hakuna ambayo ni Swahiyh zaidi kuliko hii kuhusu mada hii.”

Haya ndio maoni ya Imaam Ahmad na wanazuoni wengi wa Hadiyth. Pia yale matendo mengine yenye maana ya kupiga chuku. Kujengea juu ya hili haijuzu kwa mfungaji ambaye amefunga swawm ya lazima kujitolea damu nyingi inayoathiri mwili kama inavyofanya chuku. Isipokuwa kama amelazimika na hakuna njia nyingine na wala hakumdhuru mfungaji kule kutoa damu. Katika hali hiyo itafaa kutokana na dharurah. Lakini atakula siku hiyo na kulipa.

Kuhusu kutokwa damu puani, kwa kukohoa, bawasiri, kung´oa jino, jeraha kupasuka, damu kwa ajili ya kipimo au kudungwa sindano za kawaida hakufunguzi. Kwa sababu sio kuumika wala hakuna maana yake. Aidha hakudhoofishi mwili kama inavyofanywa chuku.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 101
  • Imechapishwa: 26/02/2024