Mume anamuomba mke acheleweshe deni la Ramadhaan

Swali: Kuna mwanamke ana deni la Ramadhaan. Anataka kulipa lakini mume wake amemuomba acheleweshe mpaka Sha´baan. Hata hivyo inajuzu kwake kulipa kabla ya hapo?

Jibu: Muda bado ukingali mpana. Ikiwa mume wake amemuomba kuchelewesha, acheleweshe. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alikuwa naye anatakiwa kulipa deni la Ramadhaan lakini anachelewesha mpaka Sha´baan kutokana na nafasi aliokuwa nayo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama ilivokuja katika Hadiyth.

Check Also

Peleka mahakamani

Swali: Mimi nina dada anayegombana na mume wake mwenye madhehebu na mfumo wa Suufiyyah. Anampiga, …