Pato la haramu kwa shangazi mgonjwa na muhitajiaji

Swali: Nilipata mali kwa njia ya haramu. Je, inajuzu kumpa nazo shangazi yangu ambaye ni fakiri na ni mgonjwa ili niweze kujinasua nazo?

Jibu: Ikiwa umetubu kwa Allaah kwa kitendo hichi mpe nazo muhitajiaji, ni mamoja ikiwa ni ndugu yako au mwingine. Unafanya hivo ili uweze kujikwamua nazo, na si kwa ajili ya kutoa swadaqah. Hii ni kama mali iliyopotea asiyopatikana mmiliki wake; mpe yule anayehitajia. Hata hivyo unatakiwa kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jall). Ama kusema uendelee kuchuma pato la haramu na kulitoa swadaqah ni haramu.

Check Also

Usimweleze muhitaji ni nani aliyempa pesa

Swali: Baadhi ya watenda wema wananipa pesa niwagawie ndugu zangu. Je, ni wajibu kuwaeleza ya …