Mume analazimika kumuhijisha mke wa pili aliyeoa ikiwa tayari wa kwanza ameshahiji?

Swali: Je, ni katika kutofanya uadilifu atapompa zawadi mmoja pasi na mwengine?

Jibu: Kinachonidhihirikia ni kwamba ni lazima kuwapa sawa baina yao katika matumizi na mfano wake.

Swali: Akioa mke wa pili na yule mke wa kwanza kishahiji naye na wa pili hajahiji kisha akasafiri na yule wa pili. Je, atalazimika kumuhijisha yule wa kwanza?

Jibu: Hainidhihirikii ya kwamba analazimika muda wa kuwa tayari ameshahiji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23899/ما-الذي-يلزم-التسوية-فيه-بين-الزوجات
  • Imechapishwa: 29/05/2024