Swali: Kuna mwanaume alimuoa mwanamke na wakazaa naye watoto wawili. Kisha akamwacha na kusafiri kwenda katika mji mwingine. Ametoa wito katika mji wake lakini hakuna mwenye kujua kitu. Inajuzu kwa mwanamke kuolewa na mwengine? Ni muda kiasi gani anatakiwa mwanaume kuwa mbali mpaka mwanamke aweze kuolewa na mwengine?
Jibu: Anazingatiwa kuwa ni mwenye kupotea; ambaye hakuna mwenye kujua khabari zake. Ikiwa pengine amefariki, hakimu atahukumu miaka mine. Na ikiwa pengine hakufa, asubiri miaka tisini tokea siku mwanaume huyo aliyozaliwa. Baada ya hapo ikipita basi hakimu atahukumu kifo chake. Kazi hii ni ya Qaadhiy. Yeye ndiye ambaye atahukumu juu ya kufa kwake sawa ikiwa inahusiana na muda mfupi au mrefu. Kukihukumiwa juu ya kifo chake basi mwanamke anatakiwa kukaa eda. Inaanza tokea siku ile mwanaume huyo amehukumiwa kufa ambapo ni miezi mine na siku kumi. Baada ya hapo eda yake imeisha na anaweza kuolewa.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
- Imechapishwa: 15/06/2020
Swali: Kuna mwanaume alimuoa mwanamke na wakazaa naye watoto wawili. Kisha akamwacha na kusafiri kwenda katika mji mwingine. Ametoa wito katika mji wake lakini hakuna mwenye kujua kitu. Inajuzu kwa mwanamke kuolewa na mwengine? Ni muda kiasi gani anatakiwa mwanaume kuwa mbali mpaka mwanamke aweze kuolewa na mwengine?
Jibu: Anazingatiwa kuwa ni mwenye kupotea; ambaye hakuna mwenye kujua khabari zake. Ikiwa pengine amefariki, hakimu atahukumu miaka mine. Na ikiwa pengine hakufa, asubiri miaka tisini tokea siku mwanaume huyo aliyozaliwa. Baada ya hapo ikipita basi hakimu atahukumu kifo chake. Kazi hii ni ya Qaadhiy. Yeye ndiye ambaye atahukumu juu ya kufa kwake sawa ikiwa inahusiana na muda mfupi au mrefu. Kukihukumiwa juu ya kifo chake basi mwanamke anatakiwa kukaa eda. Inaanza tokea siku ile mwanaume huyo amehukumiwa kufa ambapo ni miezi mine na siku kumi. Baada ya hapo eda yake imeisha na anaweza kuolewa.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
Imechapishwa: 15/06/2020
https://firqatunnajia.com/mume-amepotea-na-hajulikani-alipo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)