Mume amemuachia mkewe wasia wa kuolewa na mwanamme fulani

Swali: Kuna mtu ameacha anamuusia mke wake wakati wa kukata roho aolewe na mwanaume maalum ambaye yeye hamtaki. Je, atekeleze wasia wake?

Jibu: Hapana, asiutekeleze. Sio haki yake yeye kumuachia wasia. Mwanamke anaolewa na mwanaume anayemtaka. Asiwepo yeyote wa kumuwajibishia aolewe na mtu fulani. Hata baba yake hana haki ya kufanya hivyo pasi na ridhaa yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-08-02.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2020