Swali: Himdi zote ni za Allaah ambaye ametukusanya sehemu hii. Tunamuomba Allaah atukusanye katika mabustani ya Peponi. Hakika Yeye kwa hilo ni muweza…

Jibu: Hakika Yeye juu ya kila kitu ni muweza. Usikhusishe na kusema kuwa kwa  hilo ni muweza au ni muweza kwa yale anayoyataka. Yaeneze kama alivyosema Allaah (Jalla wa ´Alaa):

عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Hakika Yeye juu ya kila kitu ni muweza.” (41:39)

Kuhusiana na maneno ya Allaah:

وَهُوَ عَلَىٰ جَمْعِهِمْ إِذَا يَشَاءُ قَدِيرٌ

“Naye kwa kuwakusanya Atakapo ni muweza.” (42:29)

ni hali maalum ambapo Atawakusanya walioko mbinguni na ardhini siku ya Qiyaamah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-07-24_0.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2020