Muadhini anageuza uso kutoka kwenye kipaza sauti

Swali: Ikiwa muadhini anaadhini kwenye kipaza sauti ageuke wakati wa kusema:

حَيَّ عَلى الصلاةِ

“Njooni katika swalah.”

na:

حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ

“Njooni katika mafanikio.”?

Jibu: Asifanye hivo ikiwa anaadhini katika kipaza sauti. Kwa sababu inadhoofisha sauti.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/175-176)
  • Imechapishwa: 12/06/2026