Swali: Je, ni bora kumpa zakaah mdaiwa ili alipe deni lake au mwenye zakaah aende kwa yule anayemdai ili kumlipia nalo?
Jibu: Ikiwa mdaiwa huyu ni mwenye kupupia kulipa deni lake, kuitakasa dhimma yake na pia ni mwenye kuaminika, basi tutampa mwenyewe ili alipe deni lake. Kwa sababu kufanya hivo kunamsitiri zaidi mbele ya watu ambao wanamdai pesa zao. Ama ikiwa mdaiwa ni mtu mbadhirifu ambaye anafanya israfu ya pesa na endapo tutampa pesa ili alipe deni lake basi ataenda kununua vitu visivyokuwa na ulazima, basi hatutompa. Badala yake tutaenda kwa mwenye kumdai na kumlipia deni lake lote au baadhi ya deni lake.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/360)
- Imechapishwa: 12/06/2026
Swali: Je, ni bora kumpa zakaah mdaiwa ili alipe deni lake au mwenye zakaah aende kwa yule anayemdai ili kumlipia nalo?
Jibu: Ikiwa mdaiwa huyu ni mwenye kupupia kulipa deni lake, kuitakasa dhimma yake na pia ni mwenye kuaminika, basi tutampa mwenyewe ili alipe deni lake. Kwa sababu kufanya hivo kunamsitiri zaidi mbele ya watu ambao wanamdai pesa zao. Ama ikiwa mdaiwa ni mtu mbadhirifu ambaye anafanya israfu ya pesa na endapo tutampa pesa ili alipe deni lake basi ataenda kununua vitu visivyokuwa na ulazima, basi hatutompa. Badala yake tutaenda kwa mwenye kumdai na kumlipia deni lake lote au baadhi ya deni lake.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/360)
Imechapishwa: 12/06/2026
https://firqatunnajia.com/zakaah-kwa-mdaiwa/