Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kuswali swalah zote za mkusanyiko isipokuwa tu Fajr?

Jibu: Anapata dhambi kwa kuacha kuswali Fajr pamoja na mkusanyiko. Ni wajibu kwake kutubia kwa Allaah na aswali Fajr pamoja na mkusanyiko. Nachelea unafiki kwa yule ambaye hii ndio hali yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah nzito kwa wanafiki ni swalah ya ´Ishaa na swalah ya Fajr.  Iwapo wangelijua ujira unaopatikana ndani yake, basi wangeziendea ijapo kwa kutambaa.”[1]

[1] Muslim (651).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/123-124)
  • Imechapishwa: 12/06/2026