Mtume akiswali bila ya Iqaamah

Swali: Katika riwaya iliyopokelewa na Abu Daawuud imekuja kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuamuru Bilaal ambapo akakimu na akaswali kile kilichopungua?

Jibu: Riwaya mashuhuri kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa al-Bukhaariy na Muslim ni kwamba alianza swalah bila ya kukimu.  

Mwanafunzi: Ikiwa upokezi huu umesihi basi utakuwa ni dhaifu?

Ibn Baaz: Ni jambo lenye kuhitaji kuchunguzwa. Lililo karibu zaidi na sahihi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba si Swahiyh na kwamba ni dhaifu kutoka kwa baadhi ya wapokezi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27487/هل-تقام-الصلاة-مجددا-لصلاة-ما-نقص-سهوا
  • Imechapishwa: 10/04/2025