Mtume (صلى الله عليه وسلم) alizikwa nyumbani kwake

Swali: Ndani ya msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kunazingatiwa kuna kaburi?

Jibu: Hapana. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizikwa nyumbani kwake. Nyumba nje ya msikiti kisha baadaye ndipo ikaingizwa. Yaliyokatazwa ni mambo mawili:

La kwanza: Maiti kuzikwa ndani ya msikiti.

La pili: Kuujenga msikiti juu ya kaburi, jambo ambalo halikutokea kuhusu msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuzikwa ndani ya msikiti na wala msikiti haukujengwa juu kaburi. Alizikwa nyumbani kwake. Nyumba yake ilikuwa nje ya msikiti na akaiingiza ndani Waliyd bin ´Abdil-Malik kimakosa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 19/05/2019