Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
22 – Abu ‘Abdillaah Jaabir bin ‘Abdillaah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Kuna mtu alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unafikiriaje lau nitaswali swalah za fardhi, nikafunga Ramadhaan, nihalalishe halali na nikaharimisha haramu na nisifanye jambo lolote jengine nitaingia peponi? Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamjibu: “Ndio”.”
Imepokelewa na Muslim.
Hadiyth hii inaonyesha dalili ya kwamba mwenye kuyafanya mambo haya ya wajibu hali ya kuwa ni mwenye kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall), akaswali swalah za faradhi kwa kumtii Allaah (´Azza wa Jall), akafunga na kutoa zakaah kwa kumtii Allaah, akahiji kwa kumtii Allaah, akahalalisha halali na kuharamisha haramu kwa kumtii Allaah, mtu huyu ni katika watu wa Peponi.
- Muhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 310
- Imechapishwa: 27/08/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Sifa ya mtu wa Peponi
Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema: 22- Abu 'Abdillaah Jaabir bin 'Abdillaah al-Answaariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema: "Kuna mtu alimuuliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) unafikiriaje lau nitaswali swalah za fardhi, nikafunga Ramadhaan, nihalalishe halali na nikaharimisha haramu na nisifanye jambo lolote jengine nitaingia peponi? Mtume (Swalla Allaahu…
In "Ikhlaasw na ukweli"
139. Suufiyyah wenye kuonelea kwamba kuna kiwango mtu akifika anatoka katika Shari´ah
Kuna aina mbalimbali za kutoka katika Shari´ah ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuna sampuli ambazo ni kufuru na aina zengine ni kufuru ndogo. Kuna utokaji wa moja kwa moja na kutoka utokaji wa kisehemu. Wale wanaotoka katika Shari´ah au kitu katika Shari´ah hali ya kuwa wanahalalisha kitendo…
In "Sharh Nawaaqidh-il-Islaam - al-Fawzaan"
Nasaha kwa mwanamke mchaji asiyemtii mume wake
Swali: Mke wangu anaswali Nawaafil nyingi za swawm, swalah na kusoma Qur-aan. Lakini hata hivyo hajihimizi kumtii mume wake na khaswa upande wa kitandani. Naomba umnasihi. Jibu: Ninamnasihi mke wake kumtii mume wake kwa kuwa ni katika kumtii Allaah. Atekeleze haki zake na asimuasi katika wema. Atekeleze maombi yake kwa kuwa…
In "Nasaha kwa mke"