Mtu kukemea maovu njiani anapokwenda dukani

Swali: Wakati mtu anapoenda dukani mtu anaona maovu mengi. Tuchukue msimamo gani juu yake? Je, tuwakemee?

Jibu: Unajua jibu:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayakemee kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[1]

Swali: Ikiwa mtu anaweza kukemea kwa mdomo wake. Je, amkemee kila anayemuona njiani wakati anapoenda dukani?

Jibu: Unakanyaga maji. Jawabu ni lilelile:

“Yule katika nyinyi atakayeona maovu, basi ayakemee kwa mkono wake. Asipoweza, afanye hivo kwa ulimi wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”

Je, anaweza kukemea kila dhambi anayoiona njiani? Ima anaweza kufanya hivo au hawezi. Jawabu ni lilelile.

[1] Ameipokea Muslim (78), at-Tirmidhiy (2172), an-Nasaa´iy (5008) na Ibn Maajah (1275).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Raabigh (2)
  • Imechapishwa: 22/05/2021