Mtu anapokusanya faradhi mbili analeta Iqaamah kwa kila moja wapo?

Swali: Mtu akikusanya Dhuhr na ´Aswr. Je, kila kimoja katika hizo inatolewa Iqaamah yake?

Jibu: Kila moja ina Iqaamah yake. Jaabir (Rdhiya Allaahu ´anh) alipokuwa akielezea namna ya hijjah yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya kutaja ukusanyaji wake Muzadalifah kisha akasema:

“Akasimama na kuswali Maghrib, kisha akasimama na kuswali ´Ishaa na hakuleta Tasbiyh kati  yake.”

Kuhusu swalah za kujitolea hakuna baina yake Iqaamah.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/12/161)
  • Imechapishwa: 01/05/2026