Mtu ameswali pasina wudhuu´ kisha akakumbuka

Swali: Niliswali swalah za faradhi tatu bila ya wudhuu´ kwa kusahau. Je, swalah zangu ni sahihi?

Jibu: Swalah zako ni sahihi. Isipokuwa ikiwa kama umekumbuka na wakati haujatoka, kwa mfano umeswali swalah ya Fajr bila ya wudhuu´, halafu ukakumbuka kabla ya jua kuchomoza, utatakiwa wende na utawadhe kisha uswali. Ama ikiwa ni baada ya kuchomoza kwa jua, haikulazimu kuilipa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2197
  • Imechapishwa: 03/05/2015