al-Waadi´iy mwanamke kupangusa juu ya mtandio wakati wa wudhuu´

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke ambaye ameenda ili aweze kuswali katika Chuo Kikuu baada ya hapo atekeleze manufaa yake. Ametawadha na kupangusa kichwa chake juu ya Hijaab ambayo iko kichwani mwake kutokana na ugumu wa kuivua mbio mbio?

Jibu: Hakuna neno kufanya hivo – Allaah akitaka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipangusa juu ya kilemba chake kama ilivyothibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=3573
  • Imechapishwa: 03/05/2015