Mtu ambaye yuko mashghuli amemwacha imamu na kuswali kivyake

Swali: Imamu akirefusha swalah na maamuma akawa mashguli na kuna haja fulani anatakiwa kuifanya. Je, anaweza kufarikiana na imamu na kunuia kumaliza kivyake?

Jibu: Ndio. Akihitajia kufarikiana na imamu na akachelea kupotea kwa mali yake, anuie kufarikiana naye, kumaliza swalah yake kivyake na kwenda zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (91) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-22-7-1439.mp3
  • Imechapishwa: 17/08/2018