Mtu ambaye si msomi ameona faida katika Qur-aan na anataka kuieneza

Swali: Mtu ambaye si msomi akisoma Qur-aan na kuona faida awaeleze wengine au ni katika kuzungumza juu ya Allaah pasi na elimu?

Jibu: Ikiwa ni katika wanachuoni wenye kustahiki aeleze kuwa Aayah inaashiria hili na lile. Na ikiwa ni mtu ambaye si msomi ananufaika kwa kiasi na Allaah atakavyomwongoza. Hata hivyo asiwaeleze watu kwa sababu sio mwanachuoni. Anaweza kuwa amekosea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-10-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020