Kumkaba mtu shingoni wakati wa Ruqyah

Swali: Je, inajuzu kwa msomaji Ruqyah kumnyonga mwanamke wakati wa haja akisitiri shingo yake na yote haya yanafanyika mbele ya Mahram wake?

Jibu: Jini linamuudhi. Na wewe unamuudhi zaidi na kumyonga na kuyaweka maisha yake khatarini? Msomee Qur-aan. Hili linatosha. Jini litaunguzwa na kutoka lipende lisipendi. Usimpige na wala usimnyonge.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (27) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-10-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020