Mtoto wa miaka zaidi ya 7 kuingia walipo wanawake

Swali: Mtoto aliyekomaa kiasi cha kutambua mambo akiwa juu ya miaka saba, ikiwa anajua mambo ya wanawake – je, azuiwe kuingia?

Jibu: Hili linarejea kwenye maslahi na linarejea kwa mlezi. Qur-aan imesema:

وَإِذَا بَلَغَ الْأَطْفَالُ مِنكُمُ الْحُلُمَ فَلْيَسْتَأْذِنُوا كَمَا اسْتَأْذَنَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ

“Matoto miongoni mwenu watakapofikia baleghe, basi waombe idhini kama walivyoomba idhini wale wa kabla yao.”[1]

Hiyo ni baada ya kufikia baleghe. Lakini kabla ya hapo, anazuiwa katika hali tatu ambazo Allaah amezibainisha katika Suurah ”an-Nuur.”

[1] 24:59

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31689/ما-حكم-دخول-الصبي-فوق-سبع-سنين-على-النساء
  • Imechapishwa: 14/11/2025