Mtoto kuhiji kwa niaba ya aliyebaleghe

Swali: Je, inajuzu kwa mtoto kuhiji kwa niaba ya mtu ambaye kishabaleghe? Kwa maana ya kwamba mtu akamchukua mwanawe kisha akafanya hijjah ya mwanawe iwe kwa niaba ya baba yake?

Jibu: Hapana, hapana, mtoto anahiji kwa niaba yake mwenyewe hahiji kwa niaba ya mtu mwingine hadi kwanza afanye ile hajj ya faradhi.

Swali: Vipi ikiwa tayari kabla ya hapo ameshafanya hajj?

Jibu: Mpaka kwanza atekeleze hajj ya faradhi na si kabla ya hapo. Mtoto hana faradhi ya hajj hadi abaleghe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27023/هل-يجوز-للصبي-ان-يحج-عن-البالغ
  • Imechapishwa: 21/03/2025