Mtoto anawatishia wazazi wasipomuoza

Swali: Nina mtoto asiyeswali wala kufunga na umri wake ana miaka 11 na anatutishia kutuua mpaka tumuozeshe ilihali hatuna uwezo wa jambo hilo. Nifanye nini?

Jibu: Muombee kwa Allaah amwongoze. Kuhusu kumuozesha, ikiwa huwezi, basi itambulike kuwa Allaah haikalifishi nafsi yoyote isipokuwa kadri na uwezo wake. Unaweza vilevile kuwasiliana na jumuiya zinazosaidia watu wasiokuwa na uwezo wa kulipa mahari wakamsaidia juu ya jambo la kuoa. Zipo Makkah, ar-Riyaadh na kwenginepo. Hawatokufanyia mapungufu kama wanavofanya kwa wengine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Swifaat-il-Mu´miniyn https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-09/s_0.mp3
  • Imechapishwa: 24/10/2022